Nilipata bahati na fursa ya kuwatembelea kinamama waliojifungua siku ya sikukuu.niliweza kujifunza mengi sana kama ifuatavyo,
Nilidhamilia kuwatembelea watoto wachanga waliozaliwa siku ya mkesha na sikukuu,lakini sikuishia hapo niliweza kuwatembelea wagonjwa wa TB pia watoto wagonjwa lakini sikuishia hapo niliingia mpaka chumba cha watoto njiti na ni bahati kwani hairuhusiwi mtu kuingia kwenye vyumba hivyo.
kutokana na maelezo takwimu iliyo tolewa na muuguzi wa zamu ni kwamba hakukutokea kifo cha mama wala mtoto wote walijifungua salama.
Idadi ya watoto walio zaliwa takribani 26 .